YANGA SC 1-2 PYRAMIDS FC: FULL HIGHLIGHTS (CAF CC – 27/10/2019)

Wawakilishi pekee wa Tanzania kimataifa Yanga SC wamepokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Pyramids FC kutoka Misri katika mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya mtoano kombe la shirikisho barani Afrika uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Wageni Pyramids ndiyo waliotangulia kupata magoli kupitia kwa Erick Traory dakika ya 43 na Abdallah Saied dakia ya 63, na Yanga kujipatia bao lao pekee dakika ya 88 kupitia kwa Papy Tshishimbi.

Mara baada ya mchezo huo, Yanga imesema waamuzi wa mchezo wa leo wamechangia kwa kiasi kikubwa wao kupoteza mbele ya wageni wao baada ya kuonesha upendeleo kwa wageni wao Pyramids FC.

Mwandila amesema hata wao kumaliza pungufu kwa beki wao Kelvin Yondani kulambwa kadi nyekundu dakika ya 90 kumetokana na mapungufu ya waamuzi.

Lakini kwa wapinzani wao Pyramids FC wameshangazwa na uamuzi wa wenyeji wao kuamua mechi ichezwe kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Wawili hao watarudiana wiki ijayo jijini Cairo kabla ya mshindi wa jumla kuingia hatua ya makundi ya michuano hiyo.

  • Views:249,122 views
  • Categories: News