DAH! Harmonize Auza Nyumba 3 Kuwalipa WCB Milioni 500

Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars
MSANII aliyekuwa akimilikiwa na Lebo ya WCB, Harmonize amesema kuwa amelazimika kuuza nyumba zake tatu pamoja na mali zake nyingine kuilipa lebo yake hiyo ya zamani kiasi cha Tsh milioni 500 ili kuvunja mkataba nayo na kupata hakimiliki ya jina lake na kazi zake za sanaa.

Harmonize amesema hayo leo wakati akipiga stori na XXL ya Clouds FM kwenye media tour ambayo anaitangaza ngoma yake mpya ya UNO.

“Ukweli hatupo sawa na uongozi uliopita, sitaki kusema uongo, mahusiano yangu na uongozi uliopita sio kama zamani. Naomba niwashukuru kwa sababu wao ndo wamesababisha mimi kuwa hapa! Japokuwa kuna matatizo ya ndani ambayo siwezi kuyasema hadharani nimeamua kufanya kazi kama msanii huru lakini sipendi kuwavunjia heshima.

“Mkataba wangu ulikuwa unanitaka nilipe shilingi milioni 500 kama nikiondoka ili niweze kupata hakimiliki ya jina langu pamoja na nyimbo zangu. Hivyo sikuwa na hela kabisa. Nimeuza nyumba zangu tatu na baadhi ya mali, deni limebaki kidogo.

Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars

Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars

Twitter: https://twitter.com/Kidanistars